Header Ads

WATU WAPEWA LIKIZO INDIA

Rajinikanth
Image copyright
Image captionKALI ZOTE BLOG.COM
Wafanyakazi wengi kusini mwa India leo wamepewa likizo kwa sababu ya filamu ya mwigizaji filamu inayoanza kuonyeshwa kwenye kumbi za sinema leo.Filamu hiyo ni ya mwigizaji nyota wa asili ya Tamil, Rajinikanth.
Hatua hiyo imechukuliwa kuzuia watu kutumia visingizio kama vile kwamba wanaugua ili wasifike kazini.
Inahofiwa wengine huenda hata wangezima simu zao au kutofika kazini bila kueleza sababu.
Filamu hiyo kwa jina Kabali inaonyeshwa katika kumbi 12,000 za sinema leo.
Rajinikanth, ni mmoja wa waigizaji wanaolipwa pesa nyingi sana bara Asia na mmoja wa waigizaji mashuhuri zaidi kutoka India.
Hata kabla ya kuzinduliwa, filamu hiyo ya Kabali, ambayo inaangazia uhalifu wa magenge, imejizolea $30m (£20m) kupitia mauzo ya haki zake.
Itatolewa pia kwa lugha za Kitelugu, Kihindi na Kimalay.
Image copyrightGETTY
Katika miji kama vile Chennai na Bangalore, baadhi ya kampuni zimetangaza Ijumaa kuwa siku ya likizo na hata kuwapa wafanyakazi tiketi za bure wakatazame filamu hiyo.
Kampuni moja inasema imechukua hatua hiyo kuzuia watu kufika kwa wingi wakiomba likizo siku ya leo.
, mwenye umri wa miaka 65, ameigiza katika filamu zaidi ya 170, nyingi katika lugha ya Kitamil.
COPY BBC

No comments