Analipwa kubikiri watoto ili kuondoa mikosi Malawi
Katika tamaduni nyingi kote duniani mwanamke anapoolewa huwa ni fahari kubwa sana akiwa ni bikira.
Mathalan ni dhihirisho la mwanamke kuwa amelelewa na kutunzwa vyema.
Ni dhihirisho la usafi.
Hata hivyo jamii moja nchini Malawi haithamini ubikira wa watoto wao wa kike.
Amini usiamini wazazi huwa wanamlipa ''Fisi'' kumbikiri binti yao punde tu anapopata hedhi yake ya kwanza.
Wanaamini kuwa binti ambaye ni bikira ni mkosi kwa jamii!
Malimwengu haya.
Wazazi na jamii kwa jumla katika maeneo mengi ya kusini mwa Malawi wamekuwa wakishikilia tamaduni hii kwa miaka na mikaka.
''Fisi'' ama wanaume wanaowabikiri watoto wa kike huchaguliwa na wazazi kuwaondolea mikosi.
Na huwa ni sherehe kubwa inayomtangulia binti kupelekwa unyagoni kisha kuwatembelea shangazi wake kabla ya kujulishwa kwa fisi.
Amini usiamini hao mafisi hulipwa takriban dola $7 kwa kila kitendo cha ngono na hao mabinti ambao wengi huwa na kati ya umri wa miaka 11-14.
Fisi mmoja katika kijiji cha Nsanje, Eric Aniva ameiambia BBC kuwa hajui kwa kweli amewabikiri wasichana wangapi, kwa sababu ni wengi.
''Kwa kweli mimi nimewabikiri zaidi ya wasichana 104," amesema. ''Hii ndiyo tamaduni yetu''.
''Hapa mwanamke akifiwa lazima aje kwangu nimuondolee mkosi hata kabla ya kuzikwa kwa mumewe''.
''Mwanamke akiavya mimba pia kabla hajarejelea maisha yake ya kawaida ama hata kushiriki ngono na mwanamume mwengine lazima aje kwangu nimsafishe," alisema fisi huyo.
Aniva ambaye ana umri wa takriban miaka 40 ana wanawake wawili na watoto 5.
Anasema kuwa pale anaposhiriki ngono na watoto hao huwa anapewa muda wa siku 3 hivi kumsafisha na kumuondolea mkosi.
Kulingana na tamaduni zao, ikiwa mwanamke ama binti anakataa asibikiriwe huwa wanaamini kuwa jamaa zao watafuatwa na mikosi na magonjwa.
Post a Comment