Koffi Olomide adaiwa kumpiga teke mwanamke Kenya
Mojawapo wa mwanamuziki mashuhuri mkongomani Koffi Olomide,amejipata matatani baada ya kunaswa kwenye kamera akimpiga teke mwanamke, anayesadikiwa kuwa mmoja wa wachezaji ngoma wake.
Tukio hilo lilirekodiwa katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta ambako alikuwa amewasili kwa tamasha lilopangwa kufanyika nchini Kenya.
Wengi wa Wakenya wamekashifu vikali kitendo hicho huku maoni katika mitandao ya kijamii yakitoa wito watu kutohudhuria tamasha hilo na badala yake wakitaka akamatwe.
Wengine kupitia kitambulisha mada #KickKoffiOlomideBackToCongo kwenye Twitter wanapendekeza afurushwe kutoka Kenya.
Kwa upande wake Koffi Olomide, kwenye ujumbe katika ukurasa wake wa Facebook, amesema tukio hilo lilieleweka vibaya.
Amesema alikuwa anajaribu kumtetea mwanamke huyo kwani mmoja wa maafisa wa kike katika uwanja huo wa ndege alikuwa akiwasumbua wasichana hao wachezaji ngoma aliokuwa wakiandamana naye.
Katika video hiyo msichana huyo mchezaji anaonekana kukubaliana naye.
Source: BBC
Post a Comment