Header Ads

Balotelli atafute klabu nyingine

BalotelliImage copyrightREUTERS
Image captionBalotelli alikaa AC Milan msimu uliopita
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema mshambuliaji Mwitaliano Mario Balotelli anafaa kutafuta klabu mpya.
Balotelli, 25, alikaa AC Milan kwa mkopo msimu uliopita lakini amerejea Liverpool kwa mazoezi ya kabla ya msimu.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City amefungia Liverpool mabao manne tangu ajiunge nao 2014.
Image copyrightREUTERS
“Hayumo katika kiwango cha uchezaji ambapo anafaa kuwa akishindania nafasi moja au mbili na wachezaji wane au watano,” amesema Klopp.
“Kwa hivyo, ni wazi kwamba tunahitaji suluhu. Kutakuwa na klabu ambayo itakuwa na furaha kuwa na Mario Balotelli mpya."

No comments