Kozi ya waamuzi Tanzania wiki ijayo
Kozi za waamuzi wa mpira wa miguu wa Tanzania itafanyika Julai 25.Kozi hiyo itaanza moja kwa moja kwa waamuzi wenye Beji ya Fifa ambao kwa sasa idadi yao ni 18 na waaamuzi waandamizi ambao idadi yao ni 12.
Waamuzi hao na wale wanaotarajiwa kuveshwa beji hiyo, wanatakiwa kuripoti Dar es Salaam Julai 24, Mwaka huu Kabla ya kuanza kozi hiyo waamuzi wote watafanyiwa vipimo vya afya ,Wakufunzi wa kozi hiyo ni Carlos Henrique kutoka Afrika Kusini, Mark Mzengo kutoka Malawi na Felix Tangawarima wa Zimbabwe.
Baada ya vipimo, darasa la waamuzi hao litaanza kwa nadharia na vitendo. Darasa hilo litafikia mwisho Julai 29, 2016
Post a Comment