Meneja wa sasa wa klabu ya Sunderland Sam Allardyce anatarajiwa kuthibitishwa kuwa Meneja mpya wa Timu ya Taifa ya England
.Bodi ya Chama cha Soka England, kitakaa kumpitisha kama Meneja wao mpya kuchukua nafasi ya Roy Hodgson aliemaliza Mkataba wake Majuzi tu baada ya kwisha Fainali za EURO 2016 na England kutolewa kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na ‘vibonde’ Iceland.
Kwenye mchakato wa uteuzi wa wadhifa huu, Allardyce, maarufu kama Big Sam, alichuana vikali na Meneja wa Hull City Steve Bruce aliewahi kuichezea Manchester United.
Mtendaji Mkuu wa FA, Martin Glenn, alithibitisha kuwa Bodi ya Watu 12 ya FA itajulishwa rasmi kuhusu mchakato wa uteuzi wa Meneja wa Timu ya Taifa ili itoe uamuzi kwenye Kikao chao cha Alhamisi.
Waliopewa mamlaka ya kupendekeza nani atakuwa Mrithi wa Roy Hodgson ni Glenn mwenyewe, Makamu Mwenyekiti wa FA, David Gill, aliewahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Man United, na Mkurugenzi wa Ufundi, Dan Ashworth.
Aliewahi kuwa Meneja wa Man United Sir Alex Fergusonaliwaeleza wazi viongozi wa Fa kuwa Mtu pekee anayefaa wadhifa wa Meneja wa England kwa sasa ni Sam Allardyce – BIG SAM.
Post a Comment