Header Ads

Rais wa Sudan Salva Kiir, ametoa wito kwa makamu wake Riek Machar, kurejea katika mji mkuu wa nchi hiyo, Juba.

Machar

Image copyrightAFP
Image captionKALI ZOTE BLOG
Rais wa Sudan Salva Kiir, ametoa wito kwa makamu wake Riek Machar, kurejea katika mji mkuu wa nchi hiyo, Juba.
Machar, aliondoka Juba baada ya siku kadha za mapigano mapema mwezi huu kati ya wanajeshi wake na wale watiifu kwa Rais Kiir, ambayo yalisababisha vifo vya mamia ya watu.
Bw Kiir amemtaka Bw Machar kujibu ombi lake katika muda wa saa 48 na kusema atamhakikishia usalama iwapo atakubali kurejea.
Lakini Machar amesema atarejea tu Juba ikiwa kikosi huru kitatumwa mjini humo, ili kumhakikishia usalama wake.
Bw Kiir amekataa wazo la kutumwa kwa wanajeshi kutoka nje, ambalo lilikuwa limetolewa na muungano wa nchi za Upembe wa Afrika, IGAD.
Viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika pia waliidhinisha kutumwa kwa majeshi ya AU nchini Sudan Kusini.
AU inataka wanajeshi hao wawe na mamlaka zaidi kushinda kikosi cha sasa cha walinda Amani wa Umoja wa Mataifa.

No comments