Header Ads

Kiongozi wa upinzani afungwa jela C Brazaville


Image copyrightAMNESTY INTERNATIONAL
Image captionPaulin Makaya
Mahakama moja nchini Congo Brazaville imemfunga kiongozi mmoja wa upinzani kifungo cha miaka miwili jela kwa kuchochea ghasia kulingana na shirika la habari la AFP.
Mashtaka yake yanatokana na maandamano yaliokatazwa ambayo kiongozi huyo Paulin Makaya aliyapanga mwaka 2015.
Maandamano hayo yalifanywa kupinga kura ya maoni iliomaliza kipindi cha awamu mbili za kuwa raia na kumruhusu rais aliye mamlakani Denis Sassou Nguesso kupigania awamu ya pili mnamo mwezi Machi mwaka huu.
Makaya alisema kuwa ataka rufaa dhidi ya hatia hiyo huku wakili wake akiutaja uamuzi huo kuwa usio wa haki na haramu.

No comments