Header Ads

Waendesha mashtaka nchini Ufaransa wamesema watuhumiwa watano wanaotajwa kumsaidia


Image copyright
Waendesha mashtaka nchini Ufaransa wamesema watuhumiwa watano wanaotajwa kumsaidia mwanaume mwenye asili ya Tunisia kuua Zaidi ya watu themanini katika shambulio la lori lililotokea wiki moja iliyopita wamehukumiwa.
Ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu mjini Paris imesema watu watano wamehukumiwa kwa makosa yanayoshabihina na ugaidi na wako chini ya ulinzi.
Mapema waendesha mashitaka walisema mawasiliano ya simu yanaonesha kuwa muuaji, Mohamed Lahouaiej Bouhlel amekuwa akifanya mawasiliano ya kila mara na watuhumiwa wenziwe katika harakati za kupanga tukio hilo kwa miezi kadhaa.katika ujumbe ambao walijitambulisha kama askari wa Mungu na inasemekana kwamba wanahusishwa na shambulio katika ofisi za jarida la Charlie Hebdo.

No comments