Mshambulizi wa zamani wa klabu ya Chelsea ya Uingereza Demba Ba amevunjika mguu akiwa uwanjani katika mechi ya ligi kuu ya Uchina
Raia huyo wa Senegal mwenye umri wa miaka 31 alikabiliwa na mlinzi wa timu hasimu katika ligi kuu ya Uchina hapo jana Jumapili tarehe 17 Julai.
Ba ambaye anaichezea Shanghai Shenhua aligongwa na mchezaji wa timu hasimu ya Shanghai SIPG mita chache tu kabla ya kisanduku cha hatua 18, Alipoanguka mguu wake ulipinduka kwa hali isiyo ya kawaida na kuvunjika papo hapo.
Video ya mechi hiyo inaogofya haswa inavyoonesha wazi wazi mguu wake umevunjika kati ya goti na kisigono.
Kocha wa klabu yake Gregorio Manzano ameonya kuwa tukio hilo linaweza kumlazimisha nyota huyo kustaafu kucheza soka .
Post a Comment