Ratiba ya Uefa mtoano yakamilika
Timu za Astra Giurgiu, Olympiacos, Viktoria PlzeĆ, Celtic na Dinamo Zagreb zimetinga Raundi ya 3 ya Mtoano ya UEFA , baada ya kukamilika Mechi za Marudiano za Raundi ya Pili ya Mtoano.
Droo ya Raundi ya 3 ya UCL ilifanyika na kuhusisha Miamba ya Ajax, Steaua, Olympiacos, Shakhtar, Anderlecht na Fenerbahçe. Monaco iliyomaliza Nafasi ya 3 kwenye Ligi 1 huko ufaransa , na Timu za Pili za Ligi za Nchi za Ulaya ambazo ziko Nafasi za 7 hadi 15 kwenye Listi ya Ubora ya Nchi Wanachama wa UEFA.
Droo ya Pili ni kwa timu za Mabingwa iliyohusisha Washindi 17 kutoka Raundi ya Pili ya Mtoano ya UCL pamoja na Mabingwa wa ugiriki, Jamhuri ya Czech na Romania.
Washindi wa Raundi ya 3 ya Mtoano wanasonga mbele na kuingia Raundi ya Mwisho ya Mchujo ambayo ni Hatua moja kabla ya Makundi.Timu zitazoshindwa Raundi ya 3 ya Motoano zitatupwa kwenye Hatua ya Raundi ya Mwisho ya Mchujo wa UEFA ligi barani ulaya.
Post a Comment