Header Ads

Maafisa 2 wa Atlabara wameuawa Sudan Kusini


Image copyrightNO CREDIT
Image captionMaafisa 2 wa Atlabara wameuawa Sudan Kusini
Maafisa wawili wa timu ya Atlabara ya Sudan Kusini wameuawa katika machafuko yaliyotikisa mji mkuu wa Juba kuanzia Alhamisi juma lililopita.
Shirikisho la soka la Sudan Kusini limetangaza kuwa maafisa 2 wakuu wa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Sudan Kusini walipigwa risasi na watu wasiojulikana
''Bwana William Batista na Leko Nelson walipigwa risasi usiku wa kuamkia jumamosi.'' alisema mkuu wa wa SFA bwana Chabur Goc.
Image copyrightREUTERS
Image captionMapigano yamekuwa yakiendelea kwa siku kadha kati ya wanajeshi watiifu kwa Rais Salva Kiir na wanajeshi watiifu kwa makamu wa Rais Dkt Riek Machar.
Batista alikuwa katibu mkuu wa klabu hicho huku Nelson akihudumu kama meneja wa klabu hicho.
''Tunaomba mwenyezi mungu awaweke mahali pema peponi'' alisema bw Goc.
Mapigano yamekuwa yakiendelea kwa siku kadha kati ya wanajeshi watiifu kwa Rais Salva Kiir na wanajeshi watiifu kwa makamu wa Rais Dkt Riek Machar.
Image copyrightAFP
Image captionLicha ya kutia sahihi makubaliano ya amani wafuasi wa viongozi hao wawili hawajaafikiana.
Licha ya kutia sahihi makubaliano ya amani wafuasi wa viongozi hao wawili hawajaafikiana.
Vituo vya Umoja wa Mataifa pamoja na maeneo ya raia pia yameshambuliwa, jambo ambalo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linasema huenda likawa uhalifu wa kivita.
Takriban watu 200 wengi wao wakiwa wanajeshi wameuawa katika machafuko hayo.

No comments