Header Ads

Maambukizi ya kaswende na kisonono juu England


KisononoImage copyrightSCIENCE PHOTO LIBRARY
Image captionVisa vya kisonono Uingereza vimekuwa vikiongezeka
Visa vya maambukizi ya maradhi ya kaswende na kisonono nchini Uingereza vimeendelea kuongezeka, takwimu mpya zinaonesha.
Kati ya 2012 na 2015, visa vya maambukizi ya kaswende viliongezeka kwa asilimia 76 kutoka 3,001 hadi 5,288.
Visa vya kisonono navyo viliongezeka 53%, kutoka 26,880 hadi 41,193, takwimu za Afya ya Umma England zinaonesha.
Visa hivyo viliongezeka sana hasa miongoni mwa wanaume wanaoshiriki mapenzi na wanaume wenzao.
Kaswende
Image captionMtu anayeugua kaswende kabla ya kuanza kupokea matibabu
Jumla ya visa vya maambukizi ya magonjwa ya zinaa pia ilishuka kidogo na kufikia 434,456 kipindi hicho.
Visa vya kuwa na vidutu sehemu za siri hata hivyo vilishuka, jambo ambalo wataalamu wa afya wanasema huenda limchangiwa na utoaji chanjo.
Maambukizi ya chlamydia ndiyo yaliyoshuhudiwa sana, karibu nusu ya visa vya maradhi ya zinaa vilivyoripotiwa mwaka 2015 vikitokana na viini hivyo.
EnglandImage copyrightBBC WASAWAT LOKHARANG
Image captionMaafisa wa afya wanawahimiza watu kutumia kinga
Vijana sana walijitolea kupimwa kubaini iwapo wameambukizwa chlamydia lakini ni 13% ya vijana wanaume na 32% vijana wanawake waliopimwa mwaka 2015.
Genevieve Edwards, afisa wa Marie Stopes UK, amesema takwimu hizo zinafaa kuwa kama tahadhari kuhusu upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi kwa vijana na pia wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume.

VIEW BBC

No comments