Header Ads

Madonna afanya ziara Kenya

Madonna afanya ziara Kenya


Image copyrightGETTY
Image captionMwanamuziki wa POP kutoka Marekani Madonna yuko nchini Kenya kwa ziara ya kibinafsi.
Mwanamuziki wa POP kutoka Marekani Madonna yuko nchini Kenya kwa ziara ya kibinafsi.
Haijulikani alitua lini ila aliwaamkua wakenya kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter
Image captionHamjambo Wakenya ?
Hamjambo Wakenya ?
Picha hiyo ya Madonna inaonesha mbuga moja nchini Kenya!
Image captionMadonna alikutana na mkewe rais Kenyatta bi Margaret
Hapo jana alikuwa ametembelea kitongoji duni cha Kibera.
Huko alipiga picha ya hali duni ya miundo mbinu katika eneo hilo nje kidogo ya jiji la Nairobi kabla ya kuchapisha picha mbili akiwa na mwanamke mmoja aliyemtaja kama mama Sofie.
Image copyrightAFP
Image captionMadonna aligonga vichwa vya habari alipokwenda Malawi ambapo alipanga mtoto David Banda
Mara ya mwisho mwanamuziki huyo alipozuru Afrika alikwenda Malawi ambapo alipanga watoto David Banda na Mercy James.
Haijulikani haswa iwapo yuko nchini Kenya kwa shughuli sawa na hiyo.
Malkia huyo wa Pop anafahamika kote duniani kwa vibao vyake muruwa La Isla Bonita, Like a Virgin (1984), Like a Prayer (1989), Erotica (1992), Music (2000), American Life (2003),miongoni mwa vingine vingi.
Image copyrightAP
Image captionMadonna na wanawe David Banda na Mercy James.
Mwaka wa 2015, Madonna aliachilia album yenye kichwa Rebel Heart.
Madonna ana umri wa miaka 57.

via bbc

No comments