WOSIA KWENYE FAMILIA
katika jamii ya kiafrika kwa asilimia kubwa atujui umuhimu wa kuandika wosia kwa familai au mke ili badae kuondoa migogoro ambayo itatokea badae .
nadhani hata wewe ni shahidi tunaona baada ya marehem kufariki watu ushambulia mali za marehem na kuwa acha watoto katika mazingira magum na kuwa machokolaa au watoto wa mitaani
MAANA YA WOSIA
wosia ni kauli ya mwisho inayo tolewa na mtu wakati wa huai wake kwa hiali yake mwenyewe , nakuonyesha jinsi gani angependa malim zake igawanywe kwa urithi wake baadae ya kufa kwake
UMUHIM WA WOSIA
wosia uansaidia kuondoa migongano ndani ya jamii kwa sababu kila kitu kimefafanuliwa na kuelezwa bayana kuhusu mgawano wa mali husika
1.mtu anapotoa wosia anasaidia jamii inayobaki kuweza kutambua mali za marehemu
2. wosia unasaidia kuweka mjane au watoto katika hali nzuri baada ya marehem kufariki kwani mtoa wosia hawezi kumwacha mke wake amabaye walihangaika wote pasipo kumgawia mali inayo husika
3. wosia ni kitu muhim sana ambapo hata mahakama haiwezi kubadirisha yaliyomo ndani ya wosia kama yatakuwa yameandikwa bila upendeleo au ukiukwaji wa sheria iliyopo
TARATIBU ZA KUTOA WOSIA
wosia wowote ule lazima utolewe na mtu mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea.
woasia hutolewa wakati mtoa wosia akiwa na akili timamu kama ni mgonjwa aliye katika hali ya kupoteza fahamu basi asitoe wosia
;;;;; wosia wowpte lazima utolewe mbele ya mashaidi wawili au wanne idadi ya mashahidi hutegemea na aina ya wosia unaotolewa kwa masahahidi wote husuhudis kwa wakati mmojs
;;;;;wosia unapotoiewa ni muhim mke /wake wa mtoa wosia hushuhudia kuhusishwa kikamilifu
;;;warithi awapaswi kuwa mashahidi iwapo watakuwa mashaihidi basi wosia huo utakuwa batili na utakosa nguvu za kisheria
AINA ZA WOSIA
1. Wosia wa maneno
2. wosia wa maandishi
WOSIA WA MANENO
Huu hutolewa na mtoa wosia mwenyewe kwa kutamka mambo ambayo atataka yafanyike baada ya m yeye kufa. wosia huu huwa na mashahidi 4 ,amabo 2 hutoka ukoo na 2 huwa marafiki zake iwapo mtoa wosia anataka kufuta wosia wake , atawaita mashahidi wake na kufuta wosia huo kwa maneno mengine
WOSIA WA MAANDISHI
Kwa anayejua kusoma na kuandika anatakiwa atoe wosia wake kwa maandishi. wosia huu huandikwe kwa kalam ya wino au kalamu isiyofutika au ipigwe chapa .katika wosia wa maandishi tarehe ya kuandika wosia huo lazima iandikwe
;;; mashahidi wa wosia huu huwa wawili tu. mmoja anaweza kuwa rafiki na mwengine kuwa ndungu kutoka ukoo wake
;;;;nimuhim kwa mtoa wosia kuweka sahii yake na majina yake mbele ya mahahidi wake 2 anaweza pia kuweka sahii ya dole gumba la mkono wa kulia kwakuchovya wino katika kidole hicho
;;;; ni muhim mwosia kutaja jina la yule anayetaka awe msimamizi wa mali yake pamoja na anmwani yake au nambaza simu
;;;;;;wosia huu ni lazima uwe na anwani ya mtoa wosia , kijiji au kitongoji anachohishi hii huweza kusaidia katika utoaji wa wosia huo mahakamani kwa sababu yawezakana majina yanafanana na mtu mwingine ambaye naye wosia wake ulishatolewa kwa wahusika wengine
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA WOSIA
sheria inatambua na kutoa maeelekezo kuhusu masilahi ya watu wanaohusiana na wosia uliotolewa kisheria mtoa wosia hawezi kumyima mrithi wake halali/ mtoto au mtegemezi /wosia hadi hapo yafuatayo yatathibitishwa kuwa yalitendeka
[ a] mrithi anezini na mke wa mtoa wosia
[b] kujaribu kumuua mtoa wosia au kumuua mama yake
[c] kuacha kumtunza mtoa wosia wakati wanjaa na maradhi bila sababu ya msingi mtu awezi kurithisha rafiki yake sehemu ya mali yake binafi
WIKI LIJLO NITAKUFUNDISHA JISI YA KUANDIKA WOSIA KWA MANENO ENDEREA KUWA NASI
WASILIANA NASI KWA NAMBA 0742692079
Post a Comment