Header Ads

UAE KUFUNGUA UBALOZI MDOGO ZANZIBAR

Picha



SERIKALI ya Falme za Kiarabu (UAE) inatarajia kufungua ubalozi wake mdogo Zanzibar kabla ya kumalizika mwaka huu ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uhusiano wa kindugu katika nchi hizo.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi na Ushirikiano wa Kiamataifa wa (UAE), Reem Ibrahim Alhashimy alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa majadiliano kati ya viongozi wa Serikali ya Zanzibar na (UAE) Mjini Zanzibar.
Alisema kufunguliwa kwa ubalozi huo kutazidisha ushirikiano uliopo na kuongeza kasi ya utekelezaji wa yale yaliyokubaliwa baina ya nchi hizo mbili.
Waziri Reem alisema madhumuni ya kuja Zanzibar ni kuihakikishia serikali na Wananchi wa Zanzibar kwamba UAE ipo tayari kutekeleza yale yaliyoahidiwa katika ziara ya Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein iliyofanyika nchini humo mwanzoni mwa mwaka huu.
“Binafsi mimi sio mara yangu ya kwanza kuja Zanzibar nimekuwa nikitembelea kutokana na uzuri wa Zanzibar na watu wake na hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kushirikiana katika mambo yetu,"alisema.
Sekta muhimu ambazo UAE imeonesha nia ya kuisaidia Zanzibar ni pamoja na sekta ya afya, kilimo na miundombinu. Hata hivyo hakuainisha zaidi ni eneo gani kati ya Bandari na Uwanja wa ndege ambalo UAE wataweza kuisaidia Zanzibar.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Haji Gavu alisema ziara hiyo imefungua matumaini makubwa kwa Zanzibar na kwamba itasaidia Zanzibar kujikwamua kiuchumi.

ALICHOKIFANYA MANGE KIMAMBI BAADA YA WAITARA KUJIUNGA NA CCM








No comments