Zaidi ya watalii 2000 waokolewa Indonesia
Indonesia imepeleka waokoaji leo kufanya msako katika kisiwa cha utalii cha Lombok na kuwaondoa zaidi ya watalii 2,000 baada ya tetemeko kubwa la ardhi kuuwa karibu watu 98 na kuharibu nyumba elfu kadhaa.
Waokoaji walitafuta watu walionurusika leo katika vifusi vya nyumba, misikiti na shule iliyoharibiwa na maafa hayo jana Jumapili. Msemaji wa shirika la taifa la kupambana na maafa Sutopo Purwo Nugroho amesema kuna hofu kwamba idadi kubwa ya watu wamenasa katika jengo la msikiti
lililoporomoka katika kijiji cha Lading-Lading upande wa kaskazini. Ukosefu wa vifaa pamoja na barabara zilizoharibika vimekuwa vikizuia juhudi za kuwafikia walionusurika katika maeneo ya milimani kaskazini mwa kisiwa hicho, ambacho kimeathirika kwa kiasi kikubwa.
Sutopo Purwo Nugroho amesema kiasi ya watu 20,000 wamelazimika kuondoka kutoka katika maeneo yao mjini Lombok na kwamba kuna mahitaji nya dharura ya chakula na maji.
kIAPO CHA MKUU WA WILAYA YA UYUI MKOA WA TABORA
Post a Comment