Header Ads

KIFO CHA MZEE MAJUTO: Mastaa walivyomlilia

Image result for majuto



Baada ya taarifa za kifo cha Mzee Majuto kuenea kupitia mitandao ya kijamii kilichotokea leo August 8,2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili  baadhi ya watu maarufu wameonyesha kuguswa na msiba huo kupitia kurusa zao za instagram.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Ridhiwan Kikwete ameandika “Mzee Amri Athumani Baba , Rafiki na Mzee wangu Nakushukuru kwa Maisha Uliyoyaishi. MWENYEZI MUNGU Ana sababu katika Kuonyesha Upendo wake. Tunakushukuru kwa Kizazi Chako Pia…Alhaj Amri Majuto. Salamu za Pole ziende kwa Katibu Tawala Wangu wa Bagamoyo Ndg. Hamza Athumani na Nduguze wote. Tuko pamoja sana.Pumzika kwa Amani Baba Majuto


“Kazi yangu ya mwisho kama photographer/graphic designer kabla ya kwenda BBA na ndo ilikuwa mara ya kwanza kukutana na King Majuto. Mara nyingi alikuwa haji anaagiza watu wanatuma picha ila hii alikuja.”
“Nakumbuka mzee aliniambia “We dogo una vituko sana ila kituko chako kikubwa kuliko vyote ni haujui unafurahisha kiasi gani, endelea kutokujua utashangazwa”… Sidhani kama mnajua kiasi gani unajiskia ukiambiwa kitu kama hicho na mfalme. To this day nasikitika kuwa sikuwahi kumuambia alichonifanya ila naweza kumuahidi kuwa popote nitakapoenda nitahakikisha sifanyi kosa la kutokusema makubwa aliyotufanyia kama watoto wake kwenye comedy industry. FOREVER A KING 🙏🏽 inna lillahi. With respect I will never call myself KING na naomba isitokee nikaitwa pia 🙏🏽🙏🏽🙏🏽”



MILLARD AYO AMTAMBULISHA MKE WAKE REDIONI




No comments