Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 14.08.2018
Paris St-Germain wanaandaa pauni milioni 100 kwa ofa ya mchezaji wa Tottenham mwenye miaka 26 raia wa Denmark Christian Eriksen. (Express)
Schalke wana nia ya kumasaini mchezaji mwenye miaka 22 raia wa England Reuben Loftus-Cheek kwa mkopo lakini Chelsea haunda wasiruhusu kuondoka kwake. (Telegraph)
Beki wa Manchester United Matteo Darmian anataka kuondoka Old Trafford na Juventus, Napoli na Internazionale wanamwinda mchezaji huyo mwenye miaka 28 raia wa Italia. (Manchester Evening News)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho aliachanganyikiwa kufuatia madai ya Paul Pogba ya kuwepo uhusiano mbaya kati yao siku ya Ijumaa. (Telegraph)
Kipa Marcus Bettinelli, 26, anaweza akaamua kuondoka Fulham baada ya kuachwa nje ya kikosi kilichocheza mechi ya kwanza ya msimu. (Mail)
Liverpool watasikiliza ofa kwa mchezaji wa maiaka 32 mlinzi rauia wa Estonia Ragnar Klavan. (Liverpool Echo)
Kiungo wa kati wa Sunderland mwenye miaka 30 Lee Cattermole huenda akahamia Bordeaux, ambapo aliyekuwa meneja wa zamani wa Black Cats sasa ndiye meneja. (Teamtalk)
Wale wanaolengwa kuchukua nafasi ya mkurugenzi mpya wa Manchester United ni pamoja na kipa Edwin van der Sar, mkurugenzi wa Juventus Fabio Paratici na Monchi, mkurugenzi wa zamaniawa Sevilla na sasa Roma. (Independent)
Mshambuliaji Wilfried Zaha anasema bado anazungumza na Crystal Palace kuhusu kuongezwa mkataba wake huko Selhurst Park. (Mail)
Meneja wa zamani wa Argentina Jorge Sampaoli anataka kurudi kwenye usimamizi na Mexico. (Goal)
Paris St-Germain na Monaco wanataka kiungo wa kati wa Sevilla mwenye miaka 29 Mfaransa Steven Nzonzi. (France Football)
Kiungo wa kati mwenye miaka 25 Giannelli Imbula, kiungo wa kati mwenye miaka 32 msikochi Charlie Adam, winga raia wa Cameroon mwenye miaka 29 Maxim Choupo-Moting na mlinzi mwenye miaka 33 Geoff Cameron wote wana mpango wa kuondoka Stoke. (Telegraph)
Meneja wa Real Madrid Julen Lopetegui anataka kuongeza mlinzi na mshambuliaji kwenye kikosi chake kabla ya tarehe ya mwisho. (AS)
Bora zaidi kutoka Jumatatu
AC Milan wanamtafuta kiungo wa kati wa Chelsea mwenye miaka 23 Tiemoue Bakayoko kwa mkopo wa msimu wote kabla ya kumpa mkataba wa kudumu. (Sun)
Barcelona itamwinda Paul Pogba baada ya msimu wa joto wa kununua wachezaji kukamilika tarehe 31 Agosti kufuatia kukubali kuwa Manchester United hawatamuuaza mchezaji huyo mwenye miaka 25 raia wa Ufarasa mwezi huu. (Telegraph)
Kipa wa Liverpool Loris Karius, 25, anawindwa na Besiktas. Klabu hiyo wa Uturuki imekuwa na mpango wa kumsaini Mjerumani huyo kwa mkopo wa msimu wote. (Sun)
Beki wa Manchester City mwenye miaka 23 Jason Denayer amekataa kuondoka kwa mkopo kwa kuwa mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Ubelgiji anataka kuhamia klabu ya Uturuki ya Galatasaray. (Star)
Cristiano Ronaldo amewashauri Juventus kumuendea kiungo wa kati wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic. Mchezaji huyo mwenye miaka 23 raia wa Serbia amehusishwa na Manchester United na Chelsea. (Star)
Kiungo wa kati wa Paris St-Germain Adrina Rabiot, 23, amekataa ofa ya kusaini upya mkataka wake na mabingwa hao wa Ligue 1. Mkataba wa kwanza wa Mfaransa huyo unakamilika mwisho wa msimu. (L'Equipe)
Post a Comment