Kituo cha sheria na haki LHRC: Watoto 394 hubakwa kila mwezi Tanzania
Ripoti iliyotolewa na kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania imebainisha kwamba kuna ongezeko kubwa la ukatili dhidi ya watoto kwa kipindi cha miezi sita ya kwanza katika mwaka 2018.
Ongezeko kubwa la matukio ya ubakaji wa watoto ni mara tatu zaidi ikilinganishwa na kipindi cha mwaka 2017, kutoka 12 kwa mwaka hadi 533 kwa mwaka 2018.
Hivyo ni wastani wa watoto 394 wamebakwa kila mwezi katika maeneo mbalimbali ya Tanzania bara kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2018
Post a Comment