Belmadi apewa mikoba ya kuinoa Algeria
Chama cha soka cha Algeria kimemtangaza Djamel Belmadi kuwa meneja mpya wa timu ya taifa kwa mkataba wa miaka minne
Belmadi, anakuwa meneja wa sita wa Algeria katika kipindi cha miaka miwili na anachukua nafasi ya Rabah Madjer.
Belmadi aliichezea timu ya taifa ya Algeria kuanzia mwaka 2000 mpaka 2004 akicheza jumla ya michezo 20 na akifunga jumla ya 5.
Pia Golikipa wa zamani wa timu hiyo Aziz Bouras anarejea kwenye timu ya taifa baada ya kutangaza kujiuzulu mwezi Februari mwaka huu.
Post a Comment