Mwandishi aliyeshinda tuzo ya Nobel V:S: Naipaul afariki dunia
LondonFamilia ya mwandishi wa Uingereza aliyeshinda tuzo ya Nobel ya fasihi V.S. Naipaul imetangaza kwamba amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85.
Mkewe Lady Naipaul amesema amefariki akiwa amezungukwa na "wale aliowapenda baada ya kuishi maisha yaliyokuwa na ubunifu na jitihada." Naipaul aliandika zaidi ya vitabu 30 na alishinda tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka 2001.
Akiwa alizaliwa Trinidad kama mwana wa mtumishi wa umma alisomea fasihi ya Kiingereza katika Chuo Kikuu cha Oxford kama kuamua kuwa na makao Uingereza.
Lakini alikuwa akisafiri katika muda wake mwingi na taasisi ya Sweden ya kutoa tuzo ya Nobel ilimuelezea kama mtu anayezunguka dunia mno. Kazi yake ya uandishi iliangazia pakubwa mateso yaliyotokana na mabadiliko ya baada ya ukoloni.
Maafande waimbaji watuma ombi kwa Viongozi, wamtaja Rais Magufuli
Post a Comment