Uturuki kutuma ujumbe Marekani kuhusiana na suala la mchungaji
Ujumbe wa Uturuki utafanya ziara mjini Washington wiki hii kujadili mvutano unaoongezeka kati ya washirika hao wa NATO, kwa mujibu wa ripoti jana, wakati Marekani imesema nchi hizo mbili zinaendelea kutofautiana kutokana na madai yao ya msingi kwamba Ankara imwachilie mchungaji wa kanisa la kiinjili Andrew Brunson.
Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani Heather Nauert amekiri ripoti za ujumbe wa Uturuki chini ya uongozi wa naibu waziri mpya wa mambo ya kigeni Sedat Onal lakini amekataa kuthibitisha kuwapo mkutano wowote kati ya maafisa wa marekani na Uturuki.
Katika mkutano na waandishi habari Nauert amethibitisha kwamba waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo alizungumza na mwenzake wa Uturuki siku ya Jumatatu lakini amesema pande hizo mbili hazijafikia makubaliano juu ya kuachiliwa Brunson, ambaye amekuwako kizuwizini nchini Uturuki tangu Oktoba 2016.
Post a Comment