Header Ads

Mwanamke wa kwanza rubani wa ndege ya vita


Luteni Misa Matsushima.
Mwanamke mmoja nchini Japan amefuzu kuwa rubani wa kwanza wa ndege za kivita nchini humo, Luteni Misa Matsushima, mwenye umri wa miaka 26, ameanza majukumu yake leo baada ya kumaliza mafunzo ya kurusha ndege ya kivita aina ya F 15, jeshi la Japan limetangaza.


Luteni Misa amewaambia wanahabari kwamba, kwa kuwa rubani wa kwanza mwanamke atafungua fursa kwa wanawake wengine kuingia kwenye fani hiyo.
Tangu nilipoangalia sinema ya Top Gun, wakati nikiwa shule ya msingi basi nikatokea kuwapenda sana marubani wa ndege za kivita,” anasisitiza Misa.
Japan ina viwango vya juu vya ukosefu wa usawa wa kijinsia, ambapo wanawake wengi wanatarajiwa kuwa mama wa nyumbani badala ya kuajiriwa, lakini kutokana na kukabiliwa na changamoto ya kuwa na wazee wengi, mnamo mwaka 2013 Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Shinzo Abe, aliahidi kuwawezesha zaidi wanawake katika ajira.
Jeshi la Japan lilianza kuajiri wanawake kwa mara ya kwanza mwaka 1993 isipokuwa kwa marubani, ambapo iliondoa amrufuku hiyo mwaka 2015, ambapo kwa sasa wanawake wengine watatu wamejiunga kwenye mafunzo ya kuwa marubani wa ndege za kivita.

No comments