Header Ads

Rais Mstaafu akataa kuchukua malipo yake ya uzeeni



Aliyekua rais wa Uruguay Jose Mujica, aliyejulikana kama rais maskini zaidi duniani amesema hatachukua malipo yake ya uzeeni tangu aanze kuhudumu kama seneta.

Mujica aliacha kazi ya useneta mnano Jumanne, kiti ambacho amekua akishikilia tangu muda wake wa kuhudumua kama raisi ukamilika mwaka wa 2015.

Alidai kuwa amechoka na hangeweza kuendelea na kazi hadi mwaka wa 2020. Muasi huyo wa zamani wa mrengo wa kushoto ana miaka 83.

Mujica aliwasilisha barua ya kuacha kazi kwa mkuu wa seneti. Alisema ya kwamba fikra ya kuacha kazi ni ya kibinasfi huku akiongeza kuwa ni uchovu wa safari ndefu.

Hata hivyo aliongeza kua ataendelea kuchangia hoja kwa sababu bado akili yake inafanya inafanya kazi.

Mujica anayejulikana kwa matamshi yake ya kichesi aliomba msamaha kwa wenzake kwa uamuzi huo.

Mwaka 2016, alidai rais wa Venezuela Nicolás Maduro ni mwendazimu kama mbuzi.

Umaarufu wake ulienea kutokana na maisha yake ya chini ya kukataa kuishi kwenye ikulu ya rais.