Header Ads

Yanga waistaafisha jezi ya Cannavaro





Aliyekuwa beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro akiwa amevalia jezi yake nambari 23.
Kuelekea mechi maalum ya kumuaga aliyekuwa beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro, uongozi wa klabu hiyo umesema utaistaafisha jezi yake, huku wakitangaza kumpa heshima kubwa mchezaji huyo ambaye ataagwa rasmi Agosti 12 mwaka huu.
Cannavaro ataagwa mjini Morogoro ambapo kikosi cha Yanga kitashuka dimbani kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mawenzi Market inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Akizungumza na www.eatv.tv Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hussein Nyika, amesema mbali na kumuaga Cannavaro, Yanga ina mipango ya kumpeleka shule kusomea ukocha.
Hatua hiyo imekuja kutokana na heshima kubwa ambayo mchezaji huyo ameipa mafanikio makubwa klabu pamoja na timu ya taifa, Taifa Stars juu ya upambanaji wake ndani ya Uwanja”, amesema Nyika.
Cannavaro aliyekuwa akivaa jezi namba 23, jezi hiyo itastaafishwa na haitoweza kutumika tena kutokana na kumuwekea heshima mchezaji huyo ambaye amepewa wadhifa wa Umeneja wa timu kwa sasa.
Vilabu mbalimbali vimeshastafisha jezi za nyota wao kwa sababu tofauti tofauti. Manchester City walistaafisha jezi namba 23 ya Marc-Vivien Foe baada ya nyota huyo wa Cameroon kufariki uwanjani, Napoli pia walistaafisha jezi namba 10 ya Diego Maradona, Inter Milan jezi namba 4 ya Javier Zanet na vilabu vingine vingi.
Nadir Haroub amekuwa nahodha wa Yanga kwa muda mrefu tangu alipostaafu Shadrack Nsajigwa na kumwachia kitambaa ambacho na yeye anakiachia rasmi Agosti 12.



KAULI YA MWISHO YA MZEE MAJUTO KWA WANAE


No comments