Header Ads

Kenya wababe wa riadha Afrika



UK Leichtathletik-WM: Kenianer Kirui holt Marathon-Gold (Reuters/T. Melville)
Kenya ndio mabingwa wa riadha barani Afrika. Hii ni baada ya kuwazidi kwa medali Afrika Kusini na kuongoza jedwali baada ya siku tano za mashindano hayo katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja.

Kenya walimaliza na medali 11 za dhahabu, sita za fedha na shaba mbili. Afrika Kusini wao walikuwa na dhahabu tisa, fedha 13 na shaba 8. Wenyeji wa mashindano hayo Nigeria walikuwa watatu huku wakipata dhahabu 9, fedha tano na shaba tano.
Mashindano hayo yaliyohusisha timu 52 lakini hayakukosa doa kwani baadhi ya timu ziliwasili kuchelewa huku timu zengine zikilalamikia miundo mbinu duni.

No comments