Header Ads

MCHINA AUAWA NA KIBOKO WAKATI AKIMPIGA PICHA




Picha



MTALII mmoja raia wa China, Chang Ming Chuang (66) amefariki baada ya kuvamiwa na kiboko juzi jioni wakati alipokuwa akimpiga picha.
Mamlaka ya Hifadhi ya Wanyama Pori ya Kenya, imeandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Tweeter kuwa Mchina huyo alivamiwa na kiboko alipokuwa anampiga picha katika Ziwa Naivasha, eneo la Sopa Resort huko Nakuru.
 Wakati mtalii huyo akikumbwa na majanga hayo, mwenzie Wu Peng Te (62) aliyekuwa naye kwenye tukio hilo, sasa anaendelea kupatiwa matibabu kwenye hospitali zilizopo mjini hapo.

No comments