Header Ads

Mambo matano tunaweza kujifunza kutoka kwa sokwe kuhusu siasa


Chimpanzee with fingers in its ears
Kuna tofauti kati ya siasa zetu na zile za viumbe wengine waofanana na binadamu.
Profesa James Tilley amekuwa akifanyia utafiti kile tunaweza kujufunza kisiasa kutoka kwa mivutano ya mamlaka kutoka kwa makundi ya sokwe.

1. Kuwa na uhusiano wa karibu na marafiki lakini pia maadui wawe karibu zaidi

Two chimpanzees, sitting on sand,Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKuwa na uhusiano wa karibu na marafiki lakini pia maadui wawe karibu zaidi
Siasa za sokwe ni miungano inayozidi kubadilika na ikiwa utahitaji kubakia madarakani unahitaji kuwa tayari kuwageuka marafiki na kuwaenzi maadui.

2. Wakati wa kujenga miungano chagua mtu dhaifu badala ya yule aliye na nguvu

Two smiling chimpanzees sitting on a tree with arms crossedHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWakati wa kujenga miungano chagua mtu dhaifu badala ya yule aliye na nguvu
Sokwe hupanda kuwa na miungano dhaifu.
Hii inamaanisha kuwa sokwe wawili dhaifu watamuunga mkono sokwe mmoja mwenye nguvu.
Ikiwa tutafikiria hivyo basi inaweza kuwa na manufaa.

3. Ni vizuri uogopwe lakini pia ni vizuri zaidi upendwe.

Chimpanzees sitting on a rockHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNi vizuri kuwa maaarufu kwenye siasa
Viongozi wa sokwe huogopwa sana na hutawala kwa nguvu, lakini viongozi hawakai siku nyingi.
Kuwa kiongozi mwenye kufanikiwa ni lazima utafute uungwaji mkono kutoka kwa wengi na kuwa mkarimu ndio suluhu.

4. Ni vizuri kupendwa, lakini pia ni vizuri zaidi kutoa vitu kama zawadi

Three chimpanzees sit in a group appearing to have a meetingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionChukua hii rafiki yangu
Viongozi wanaotawala kwa muda mrefu ni wale huchukua mali na kuitumia mali hiyo kununua uungwaji mkono.

5. Vitisho vya nje vinaweza kuchangia uungwaji mkono (ikiwa ni vya kweli...)

Chimpanzee family is sitting in a treeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWakati kuna vitisho vya kutoka nje, makundu ya sokwe huja pamoja na kupambana kwa pamoja.
Wakati kuna vitisho vya kutoka nje, makundu ya sokwe huja pamoja na kupambana kwa pamoja.
Isipokuwa hili hufanyika tu kwa binadamu kama kuna tisho lisilotarajiwa kama mashambulizi ya 9/11

No comments