Header Ads

Komu afunguka kutimkia CCM


Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini (CHADEMA), Anthony Komu.
Akizungumza na East Africa BreakFast ya East Africa Radio amesema kuwa hawezi kuondoka CHADEMA na hajawahi kufanya mazungumzo na Waitara kuhusu suala hilo kwani yeye ndio muasisi wa upinzani na anajivunia historia hiyo .
Mimi sio sehemu ya mpango huo na sielewi Waitara katoa wapi taarifa hiyo naomba wananchi wangu watambue kuwa mimi sio mpinzani wa kuunga unga mimi ni miongoni mwa waasisi wa upinzani”, amesema Komu.
Jumamosi ya Agosti 11, 2018 kupitia Weekend BreakFast ya East Africa Radio Waitara aliwataja wabunge watano kutoka CHADEMA wanaotaraji kujiunga na CCM akiwemo Anthony Komu.
Msikilize hapo chini Komu amefunguka zaidi.

No comments