Header Ads

Saudi Arabia yasitisha safari za ndege

Sitisho hilo litaanza siku ya Jumatatu ya wiki ijayo
Shirika la ndege la Saudi Arabia liitwalo Saudia Airline limesema litasimamisha safari zake kwenda mji wa Toronto Canada kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo.
Hatua hii inakuja baada ya mgogoro baina ya pande hizo mbili kudumu kwa muda mrefu.
Mapema waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Adel al-Jubeir alitangaza uhusiano baina ya nchi hizo mbili kuzorota
Saudia pia imemfukuza balozi wa Canada nchini humo sambamba na kuondoa mabadilishano yote ya elimu yaliyokuwepo baina ya pande hizo mbili.

    Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje wa Canada Chrystia Freeland nchi yake siku zote itasimamia haki za binaadam pamoja na haki za wanawake.
    Siku ya Ijumaa, Canada ilielezea kusikitishwa kwake baada ya kukamatwa kwa wanaharakati nchini Saudi Arabia, miongoni mwao akiwemo mwanaharakati maarufu Samar Badawi huku Canada ikitaka kuachiliwa kwao mara moja.
    Riyadh inasema haikubali na kamwe haitakubali kuingiliwa kwa mambo yake ya ndani.

    No comments