Wanajeshi watano wa kenya wauawa katika mlipuko barabarani
Wanajeshi watano wa Kenya wameuawa jana, baada ya gari lao kulipuliwa na kilipuzi cha kutegwa ardhini, mashariki mwa jimbo la Lamu. Duru za polisi zimesema.
Afisa mmoja mkuu wa polisi katika jimbo la Lamu ambaye hakutaka jina lake litambulishwe, amesema wanajeshi hao walikufa papo hapo baada ya kilipuzi kuripuka na kuliharibu gari lao vibaya . Wanajeshi wengine 6 walijeruhiwa.
Afisa mwengine wa polisi katika kaunti ya Lamu amethibitisha vifo hivyo lakini hakutoa maelezo zaidi. Shambulizi hilo ambalo polisi imelaumu kufanywa na wanamgambo wa kundi lenye mafungamano na al-Qaeda, la Al-Shabaab, lilifanyika barabarani katika mji wa Bodhei karibu na msitu wa Boni, ambao wanamgambo hao wa Kiislamu hujificha.
AELEZEA JUU YA IDIAMINI WALIVYO TEKWA
Post a Comment