Header Ads

Facebook na Instagram zazindua programu itakayodhibiti muda wako katika mitandao hiyo

Facebook na Instagram zinazindua programu mpya itakayodhibiti muda unotumiwa na wateja wao katika programu hizo.
Picha ya mtumiaji wa facebook


Programu hiyo itapatikana katika ukurasa wa mipango ama settings katika programu zote mbili kupitia kubofya "Your Activity" katika Instagram ama "Your Time katika Facebook"
Tangazo hilo linajiri kufuatia malalamishi kwamba utumizi wa muda mrefu unaweza kuathiri vibaya afya ya akili.
Watumiaji sasa wataweza kuona kiwango cha muda waliotumia katika mitandao hiyo miwili na kujikumbusha muda waliofikia ili kufunga ujumbe wanaopata kwa muda fulani.
''Lakini baadhi ya watu wanasema kuwa haitoshi. Siwezi kusema kuwa ni mabadiliko makubwa ama iwapo itabadilisha mambo mengi kuhusu vile watu wanavyotumia facebook ama Instagram'', alisema Grant Blank kutoka kwa taasisi ya Oxford.


Picha za FacebookHaki miliki ya pichaFACEBOOK
Image captionProgramu hiyo itapatikana katika ukurasa wa settings katika programu zote mbili kupitia kubofya "Your Activity" katika Instagram am "Your Time katika Facebook"

Facebook ilichapisha chapisho la blogi mwezi Disemba 2017 ambalo lilitambua athari mbaya za kutumia mtandao miongoni mwa wateja wake.
Katika jaribio moja , wanafunzi katika chuo kikuu cha Michigan ambao wailoambiwa kuingia katika mitandao yao ya facebook kwa dakika 10 walisalia na hali mbaya mwisho wa siku ikilinganishwa na wale waliotakiwa kuingia mara kwa mara katika mitandao hiyo-wakichapisha ama kuzungumza na marafiki zao.

No comments