Rais dkt john pombe magufuli amesema amebaini uingizwaji wa makontena ishirini kila siku ya sukari
Rais dkt
john pombe magufuli amesema amebaini uingizwaji wa makontena ishirini kila siku
ya sukari ya magendo katika mpaka wa sirali mkoani mara.
Akizungumza
na vyombo vya habari ikulu jijini dar es
salaam mara baada ya kutoka katika mazungumzo ya faragha na mgeni wake rais wa
Uganda yoweri mseven amesema kuwa tayari
ameshawaagiza mawaziri husika kwenda kufuatilia tatizo na kuchukua hatua
zinazostahili.
Rais dkt
john pombe magufuli amesisitiza pia kuwa mahusiano ya Tanzania na Uganda yapo
imara na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na nchi hizo ukiwemo mradi wa
ujenzi wa bomba la mafuta gaph kutoka hoima nchini Uganda hadi tanga Tanzania
unaendelea vizuri.
Kwa upande
wake raisi yoweri mseveni wa Uganda amesema pamoja na mambo mengine amekuja
kumpa taaarifa ya mkutano wa BRICS uliofanyika nchini afrika ya kusini.
Raisi
Magufuli amekutana na rais mseveni wa Uganda ambaye ametembelea Tanzania kwa
ziara ya kikazi ya siku moja
Post a Comment