Watu sita wauwawa katika shambulizi la waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
KinshasaDuru za kiraia na kijeshi zimesema watu sita wameuwawa katika shambulizi linalodaiwa kutekelezwa na waasi wa Uganda wa Allied Democratic Forces, ADF mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Kiongozi wa eneo la Beni, Donat Kibwana ameliambia shirika la habari la AFP waasi wa ADF waliingia katika mji wa Mayi-Moya na kuwauwa watu hao sita na kumjeruhi mtu mwengine.
Kulingana na msemaji wa jeshi Mak Hazukay watu hao sita waliuwawa kwa kuchomwa visu baada ya waasi hao kuepuka sehemu walizokuwa wanajeshi. Uongozi unasema wakaazi wa Mayi-Moya wameanza kuondoka mji huo na kutafuta sehemu salama kwa hofu ya mashambulizi zaidi.
ADF ni kundi la wanamgambo lililoundwa na waasi wa Kiislamu wanaompinga Rais wa Uganda Yoweri Museveni ila linafanya harakati zake katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo pia. Wamekuwa mashariki mwa jamhuri hiyo tangu mwaka 1995 na wamelaumiwa kwa msururu wa mauaji ya mamia ya watu.
chanzo dw swahili
kauli ya rowasa kwa walio ama chadema kuamia ccm
Post a Comment