IJUE EBOLA ,DALILI ZAKE,MAAMBUKIZI NA NJIA ZA KUJIKINGA
EBOLA ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ambavyo uishi katika miili ya binadamu na wanyama. Kwa mara ya kwanza ugonjwa huu ulitokea mwaka 1972 katika milipuko miwili iliyotokea kwa pamoja katika sehemu ya Nzara nchini Sudan na Yambuku nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo karibu na mto Ebola ambapo jina la ugonjwa huu lilipatikana. Toka kipindi hicho kumekuwa na muendelezo wa milipuko mbalimbali katika nchi tofauti za Afrika katika miaka tofautitofauti.
Mlipuko wa sasa wa ugonjwa wa Ebola umetokea katika nchi zilizopo magharibi mwa Afrika ,kesi ya kwanza iligunduliwa mwezi Machi,2014. Mlipuko wa sasa ni mkubwa zaidi kuwahi kutokea toka virusi wasababishao ugonjwa huu ulipogunduliwa mwaka 1976 ukiwa umesababisha vifo vingi zaidi kuliko milipuko yote ya miaka ya nyuma kwa pamoja.Mlipuko wa sasa umeathiri nchi nyingi zaidi,miongoni mwa nchi zilizoathrika sana ni Guinnea,Sierra Leone na Liberia.Kutokana na mlipuko wa sasa kuwa na athari kubwa na kuathiri nchi Zaidi mnamo Agusti 8,2014 shirika la afya ulimwenguni (WHO) lilitanganza mlipuko huu kuwa ni dharura ambayo nchi zote duniani zilitakiwa zishiriki katika harakati za kuudhibiti.
DALILI ZA UGONJWA WA EBOLA
Dalili za ugonjwa wa Ebola huaanza kuoneekana siku 2 mpaka 5 tangu mtu apate maambukizi ila kwa wastani ni siku 8 mpaka 10.
Zifuatazo ni dalili kuu za ugonjwa wa Ebola;
- Homa
- Maumivu makali ya kichwa
- Maumivu ya misuli
- Kufa ganzi
- Kuharisha
- Kutapika
- Maumivu ya tumbo
- Kutokwa damu pasipo sababu sehemu mbalimbali za mwili
Unapoona dalili moja au zaidi kati ya hizi unatakiwa uwahi mara moja katika kituo cha afya kwa uchunguzi Zaidi na matibabu itakapohitajika.
NJIA ZA MAAMBUKIZI YA EBOLA
- Ugonjwa wa Ebola usambazwa kwa njia ya kugusa majimaji ya mwili wa mgonjwa au mnyama aliyeathiriwa na ugonjwa huu. Majimaji yatokanayo na damu,kinyesi na matapishi yanasababisha maambukizi kwa kiasi kikubwa.
- Virusi vya Ebola pia hupatikana katika maziwa ya mama,mkojo na shahawa.Virusi huendelea kupatikana kwa siku 70 hadi 90 kwenye shahawa za mwanaumme aliye na ugonjwa huu.
- Machozi na mate pia yanaweza kuwa na virusi vya ugonjwa huu
- Virusi vya Ebola pia vinaweza kusambazwa kwa njia ya kugusa sehemu na vitu kama meza,vitinda na kadhalika ambavyo vina virusi tayari.
- Virusi vya Ebola mara nyingi havisambazwi kwa njia ya hewa ila vinaweza kusambaa kwa njia ya matone ya majimaji yanayotoka kinywani au puani pale mgonjwa anapokohoa au kupiga cha fya.
NJIA ZA KUJIKINGA NA EBOLA
- Hakikisha usafi wa mwili wako, kwa mfano osha mikono yako kwa maji safi na sabuni na epuka kugusa damu au majimaji ya mtu yeyote.
- Usiguse vitu kama nguo,shuka,vifaa vya matibabu na kadhalika ambavyo vimeguswa na damu au majimaji ya mgonjwa wa Ebola
- Epuka kushiriki mazishi ambayo yanahusisha kugusa mwili wa mtu aliyefariki.
- Epuka kugusana na popo na wanyama jamii ya sokwe au majimaji,damu na nyama zao .
- Epuka kusogelea sehemu zilizotengwa kwa ajili ya matibabu ya wagonjwa wa Ebola
- Baada ya kutoka eneo lenye mlipuko wa ugonjwa huu fuatilia kwa umakini afya yako kwa kipindi cha siku 21 na ukiona dalili zozote za ugonjwa huu nenda kituo cha afya mara moja.
NJIA ZA KUJIKINGA KWA WATOA HUDUMA ZA AFYA
Wahudumu wa afya ni miongoni mwa watu walio katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya ugonjwa huu kutokana na ukaribu walionao na wagonjwa.Kutokana na hali hiyo Wahudumu wa afya wanatakiwa kuwa makini sana wanapotoa huduma kwa wagonjwa.
- Vaa nguo zinazotakiwa za kujikinga na maambukizi
- Tenga wagonjwa wa Ebola na wagonjwa wengine
- Epuka kugusa moja kwa moja bila kinga miili ya watu waliofariki kutokana na Ebola
- Ikitokea umegusa moja kwa moja majimaji,damu,mkojo,machozi au shahawa za mgonjwa wa Ebola toa taarifa haraka kwa afisa wa afya.
Post a Comment