Jezi namba 23 ya Cannavaro kustaafishwa Yanga ?
Kushoto ni Nadir Haroub 'Cannavaro' akiwa na msemaji wa Yanga Dismas Ten.
Klabu ya Yanga imeeleza kuwa maandalizi ya mchezo wa bonanza dhidi ya Mawenzi FC ya Morogoro utakaopigwa Agosti 12, ukiwa ni maalum kwa kumuaga nahodha wao Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye amestaafu yamekamilika.
Taarifa kutoka idara ya mawasiliano ya Yanga zimeeleza kuwa, kumekuwa na maswali na maoni mengi ya wanachama na mashabiki kuhusu jezi namba 23 ambayo huivaa Cannavaro ambaye anastaafu. Wengine wakitaka istaafishwe na uongozi umesema unalifanyia kazi suala hilo na siku ya mchezo wataweka wazi hatma ya jezi hiyo.
Mbali na suala la jezi namba 23 ambayo Cannavaro ameivaa tangu mwaka 2006 alipojiunga na timu hiyo, pia wameeleza kuwa bonanza hilo litakuwa na burudani ya wasanii mbalimbali na tayari wameshamalizana nao hivyo watakuwepo kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Vilabu mbalimbali vimeshastafisha jezi za nyota wao kwa sababu tofauti tofauti. Manchester City walistaafisha jezi namba 23 ya Marc-Vivien Foe baada ya nyota huyo wa Cameroon kufariki uwanjani, Napoli pia walistaafisha jezi namba 10 ya Diego Maradona, Inter Milan jezi namba 4 ya Javier Zanet na vilabu vingine vingi.
Nadir Haroub amekuwa nahodha wa Yanga kwa muda mrefu tangu alipostaafu Shadrack Nsajigwa na kumwachia kitambaa ambacho na yeye anakiachia rasmi Agosti 12. Tayari Cannavaro ameshakabidhiwa majukumu mapya ndani ya Yanga ambayo ni kuwa meneja wa timu
kIAPO CHA MKUU WA WILAYA YA UYUI MKOA WA TABORA
Post a Comment