Header Ads

Baba ajiweka tatoo kufanana na mwanawe aliyefanyiwa upasuaji


Baba ajiweka tatoo kufanana na mwanawe aliyefanyiwa upasuaji

Image captionBaba na mtoto
Baba wa miaka 28 nchini Marekani amenyoa kichwa chake na kuweka mchoro wa tatoo unaofanana na kovu la kichwa cha mwanawe aliyefanyiwa upasuaji.
Josh Marshall,ambaye anatoka Kansas aliingia katika shindano la kila mwaka linaloendeshwa na shirika la hisani kuhusu saratani ya watoto na kushinda taji la #BestbaldDad{baba mwenye kipara kizuri} wikendi iliopita.
Akikiri aliandika: Mimi na mwanangu katika hafla ya St. Baldtricks huko Wichita Kansas.
Niliwekwa tatoo ya kovu la mwanangu ili kuimarisha motisha yake.
Shindano hilo huwashirkisha watu wa familia na marafiki wa mtoto aliye na saratani.
Image captionBaba na mwanawe
Mwanawe alipatikana na uvimbe katika ubongo mnamo mwezi Machi.
''Mwanangu alikuwa na wasiwasi mwingi baada ya kufanyiwa upasuaji,alijihisi kama hayawani'',alisema Josh Marshal.

No comments