David Rudisha ni 'afande' Kenya
David Rudisha ni 'afande' Kenya
Je wajua kuwa bingwa wa dunia wa mbio za mita 800 za wanaume David rudisha ni afisa mkuu wa polisi nchini Kenya? maelfu ya mashabiki wake walipigwa na butwaa alipochapisha picha yake akiwa amevalia sare rasmi ya kikosi cha utumishi kwa wote katika ukurasa wake wa mtandao wa Facebook.
Picha hiyo inayomuonesha akiwa amevalia sare ya kikosi cha polisi inadhihirisha kuwa ni afisa wa ngazi ya juu.
Sio aghalabu kuwa bingwa huyo na mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mita 800 kwa upande wa wanaume ni afisa polisi, asilimia kubwa ya wanariadha wakenya ni maafisa wa idara mbali mbali za vikosi vya ulinzi.
Hata hivyo hii ndio mara ya kwanza kwao kumuona Rudisha akiwa nadhifu na mtumishi kwa wote.
Wakenya wengi walisambaza picha hiyo katika mitandao ya kijamii.
Wengine walimuuliza iwapo 'Afande'' huyo pia anapokea mlungula kama maafande wengine wa kitengo cha kuongoza magari cha 'Trafiki' kama ilivyobainishwa katika uchunguzi wa maadili unaoendelea nchini Kenya.
Hata hivyo Rudisha alichapisha ujumbe huo akiwarai mashabiki wake kote duniani wajivunie kazi zao.
''Nafahamu kuwa wengi wenu mumezoea kuniona nikiwa nimevalia jezi zangu za riadha , lakini hivi ndivyo ninavyovaa nikiwa nje ya viwanja vya riadha !
Najivunia kuwa afisa wa polisi! #Loveyourjob''
Rudisha amewahi kupata umaarufu mkubwa nchini kenya hususan alipovunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 800.
Aidha ametumika katika matangazo mengi tu ya kibiashara.
from bbc
Post a Comment