Wabunge wakaa chini shinikizo la silaha
Wabunge wakaa chini shinikizo la silaha
Wabunge wa chama cha Democrats huko Marekani wamegoma kukaa kwenye viti vya bunge la Congress la nchi hiyo na kukaa kwenye sakafu kushinikiza kutungwa kwa sheria kali kuhusu umiliki wa bunduki.
Wanataka Bunge hilo kuendelea na vikao vyake vilivyopangwa hadi wiki ijayo ili wapigie kura sheria hiyo kufuatia mauaji yaliyotokea katika klabu ya usiku huko Florida.
Hata hivyo Spika wa Bunge hilo Paul Ryan, kutoka chama cha Republican ametupilia mbali hatua hiyo ya kukaa sakafuni kusema hiyo ni mbinu ya kujitangaza kisiasa.Mbunge mmoja wa Democrat Jared Huffman kutoka California amempinga spika huyo na kumtaka afanye kazi na wabunge wa Democrats.
"Spika Ryan, toka nje ya ofisi yako. Njoo uzungumze na sisi. Sikiliza sauti ya raia wa Marekani. Jiondoe kwenye mlengo wa kulia kwa ajili ya maslahi maalum yasiogemea upande wowote wa itakadi na kusikiliza sauti ya raia wa Marekani. Kama hatuna mswada, kama hatutapiga kura hatutakuwa na mapumziko.Naye mbunge mmoja John Lewis amesema maisha ya maelfu ya watu wasio na hatia yamepotea, lakini bunge hilo halijafanya chochote.
""Muda wa kunyamaza kimya na uvumilivu umekwisha. Tunataka uongozi wa bunge waje na mswada wa sheria wenye maana hapa bungeni wa kudhibiti bunduki. Tunataka kupiga kura. Turuhusu tupige kura. Tumekuja hapa kufanya kazi yetu. Tumekuja hapa kufanya kazi Raia wa marekani wanataka hatua zichukuliwe."
Post a Comment