Mtanzania aapata shavu klabu ya Dubai
Mwanariadha wa Tanzania katika eneo la Mianzini,huko Arusha Michael Gwandu amesaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Al Nasri ya Dubai kuiwakilisha kwa shindano la miruko mitatu yaani triple jump.
Asema mfuko wake sasa una uzito tofauti na miaka iliyopita akisota mjini Arusha.
''Nimezaliwa Arusha miaka 22 iliyopita.Nilianza kushiriki mashindano ya shule mwaka 2011''.
Pia anasema kuwa ameshiriki mashindano ya taifa kuanzia mwaka 2011 na kuwa bingwa mara zote katika michezo ya triple jump na long jump.
Gwandu ameongezea kuwa amewahi kuwa bingwa wa mashariki na kati katika mchezo wa Long Jump 2011 hadi 2013.
Mnamo mwaka 2015 alipata mualiko kwenda Dubai ambapo alijishindia medali ya fedha katika mchezo wa long jump silver na medali ya dhahabu katika mchezo wa triple jump.
Post a Comment