Mamelodi Sundowns yaichapa Enyimba
Mamelodi Sundowns yaichapa Enyimba
Klabu ya soka ya Mamelodi Sundowns ya Afrika kusini imeichabanga Enyimba ya Nigeria mabao 2-1 mjini Pretoria katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika siku moja baada ya vigogo wengine wa Afrika Al Ahly kuambulia kichapo nyumbani dhidi ya Asec Mimosas.
Kabla ya mchezo huo Sundowns waliwafunga Entente Setif ya Algeria 2-0 lakini mchezo huo ukatangazwa batili baada ya Setif kushindwa kuwazuia mashabiki wao kufanya fujo.
Ushindi huo unaipa Sundowns alama sawa na Zamalek katika kundi B timu zote zikiwa na ushindi wa mchezo mmoja huku zikiwa zimesalia timu tatu katika kundi hilo.
Enyimba wanaburuza mkia wakiwa bado hawajapata alama yoyote katika michezo yao ya ufunguzi.
Post a Comment