Klabu ya Yanga yalazwa nyumbani
Klabu ya Yanga yalazwa nyumbani
Klabu ya TP Mazembe iliilaza Young Africans Yanga ya Tanzania 1-0 siku ya Jumanne katika kombe la shirikisho ili kujipatia ushindi wake wa kwanza ugenini katika shindano la vilabu bingwa Afrika mwaka huu.
Timu hiyo ya DR Congo ilifunga bao lake kunako dakika ya 75 nchini Tanzania wakati Mervielle 'Bope' Bokadi alipofunga akiwa karibu na goli kutokana na pasi muruwa ya Roger Assales.
Mazembe ikiwa ndio timu iliofanikiwa zaidi katika CAF ilishushwa daraja baada ya kuondolewa na Wydad.
Ushindi wao nchini Tanzania ,katika uwanja uliojaa mashabiki kufuatia hatua ya kuwaacha mashabiki kuingia bure unaiweka timu hiyo kumaliza juu ya kundi A.
Post a Comment