Mkewe rais wa Marekani bi Michelle Obama amejiunga na mtandao wa kijamii wa Snapchat.
Mkewe rais wa Marekani bi Michelle Obama amejiunga na mtandao wa kijamii wa Snapchat.
Bi Obama alitangaza kujiunga na Snapchat siku chache kabla ya kufunga safari ya Afrika ambako anatarajiwa kujiunga na wanaharakati wa naopigia debe elimu ya mtoto wa kike .
Ziara hiyo ya itampeleka Liberia, Morocco na kisha Uhispani.
Mtandao huo unamruhusu kujumuika na walengwa wa mradi huo wa vijana.
Snapchat ni mtandao unaoruhusu habari picha na video kutoweka au kufutika baada ya saa 24.
Bi Obama alichapisha picha yake mwenyewe na kutangaza kuwa sasa amejiunga na kuwa yeye ni mmoja wao!
Mmoja wa maafisa katika afisi yake Kelsey Donohue, alizungumzia kujiunga kwake na Snapchat .
Wachanganuzi wanatarajia Bi Obama kupata wafuasi maradufu haswa mashabiki wake ambao wanatarajia kuona picha za ndani ya ikulu ya White House na pia kitaru chake kidogo mbali na habari kuhusiana na kampeini yake mpya ya
Let's Move!
Bi Obama atajiunga na wasanii Meryl Streep na Freida Pinto katika ziara hiyo barani Afrika.
Wanawe Malia na Sasha wataambatana na mama yao katika ziara hiyo.
Mkewe Obama anawafuasi 4.58m kwenye mtandao wa Twitter na 5m kwenye mtandao wa Instagram.
Post a Comment