Kamati ya Olimpiki kujadili marufuku ya Urusi
Kamati ya Olimpiki duniani IOC inatarajiwa kujadili kauli tata la Urusi kupigwa marufuku kushiriki mashindano yeyote ya riadha duniani na shirikisho la riadha duniani IAAF.
Wandani wanatarajia kamati hiyo ya Olimpiki ambayo kimsingi ndiyo inayoendesha michezo ya Olimpiki kuratibu kauli hiyo ya IAAF dhidi ya wanariadha wa Urusi.
Juma lililopita IAAF ilikataa kuondoa marufuku dhidi ya wanariadha wa Urusi ikisisitiza kuwa serikali ya nchi hiyo imekuwa ikiendesha mpango unaohujumu juhudi za shirika la kupambana na matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu mwilini WADA za kubaini kiini hasa cha idadi kubwa ya wanariadha kutoka Urusi kupatikana na hatia ya kutumia madawa hayo haramu.
Kutokana na hilo Kamati kuu ya Olimpiki Duniani- IOC, inatarajiwa kuelezea leo kwamba wanariadha wa Urusi wamezuiwa kushiriki katika mashindano ya mwaka huu ya olimpiki huko Rio- Brazil.
Wanariadha hao wanatuhumiwa kutumia madawa za kuongeza nguvu mwilini.
Kamati hiyo ya Olimpiki hata hivyo ina uwezo wa kubatilisha uamuzi wa IAAF uliokashifiwa na rais wa Urusi Vladimir Putin kuwa haikuwa ya haki haswa kwa wanariadha wa Urusi ambao hawajawahi kupatikana na hatia hiyo.
Katika mkutano huo wa Lausanne nchini Uswisi, kati ya mamlaka ya kuchunguza matumizi ya dawa za kusisimua misuli WADA na IOC pamoja na shirikisho linalo simamia riadha duniani IAAF , hoja ya kuwaruhusu wanariadha kutoka urusi watakao fanyia mazoezi yao nje ya nchi hiyo na kufanyiwa uchunguzi na WADA kushiriki katika mashindano hayo ya Rio itajadiliwa.
Aidha mbinu ya kukabiliana na mataifa mengine yaliyokiuka kanuni za WADA kama vile Kenya pia itajadiliwa.
Post a Comment