Header Ads

wakazi wa masekero watimuliwa vumbi

wakazi wa kata ya masekero katika manispaaya shinyanga leo walifunga barabara wakishinikiza kampuni ya JASCO AMBAYO inapitisha magari makubwa yanayosomba mchanga kuepuka mwendo kasi hali inayotushaia usalama wao


majira ya saa moja asubuhi wananchi hao kwa kushirikiana na viongozi wao walifunga barabara ya masekelo kwa zaidi ya masaa sita wakiweka magogo,mawe pamoja na kamba wakizuia magari ya kampuni ya JASCO  inayoshughulika na ujezi wa barabara za rami mjini shinyanga , kwa madai kuwa yanaendeshwa kwa mwendo kasi .vilevile kutimua vumbi

wamezitaja athari  zinazowapata kutokana na vumbi linalosababishwa na magari ya kampuni hiyo kuwa ni kuungua kifua kikuu ,kikohozi,lakini pia usalama waouko hatarinikwani mwendo kasi ,wa magari unaweza kusababisha vifo visivyo kuwa vya lazima 

akizungumza diwani suala hilo bwana SAMWEL SAMABAI amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa lengo  ni kushinikiza kampuni hiyo kusitisha kilio cha wananchi ambao wanaathirika , kwani licha ya kufikisha malalamiko yao ngazi ya halmashauri lakini pia katika kampuni hiyo ya JSCO ,lakini hakuna hatua zozote

mwandisi mkuu wa kampuni ya JASCO  VASANTH KUMAR amekiri kupokea malalmiko ya wakazi wa kataya masekero na ameahidi kuyapatia ufumbuzi wa haraka ili kuondoa kero kwa wananchi na kampuni iweze kuenderea na kazi

No comments