Croatia Timu ya Croatia imeichapa Hispania jumla ya magoli 2 - 1 katika mchezo wa kusisimua wa kundi D wa michuano ya Kombe la mataifa ya Ulaya Euro inayochezwa huko Ufaransa.
Timu ya Croatia imeichapa Hispania jumla ya magoli 2 - 1 katika mchezo wa kusisimua wa kundi D wa michuano ya Kombe la mataifa ya Ulaya Euro inayochezwa huko Ufaransa.
Hata hivyo timu zote Croatia na Hispania zimesonga mbele katika hatua ya 16 kutokana na kushika nafasi mbili za juu za kundi D.
Katika mechi nyingine ya kundi D iliyochezwa sambamba na hiyo Uturuki imeadhibu Jamuhuri ya Czech kwa jumla ya magoli 2 - 0.
Pamoja na ushindi huo timu zote mbili zimetolewa.
Tayari timu kumi na mbili zimeshafuzu katika hatua ya 16 ambazo ni kama ifuatayo:
Kundi A: Ufaransa na Uswis
Kundi B: Wales na England
Kundi C: Ujerumani and Poland
Kundi D: Uhispania and Croatia
Kundi E: Italy
Kundi F: Hungary
Nyingine zilizofuzu ni Ireland ya Kaskazini ambayo imesonga mbele kwa kushika nafasi ya tatu bora (best looser) kwenye kundi C na Slovakia ambayo nayo imeshika nafasi ya tatu bora kwenye kundi B.
Post a Comment