Taifa la Albania limesema kuwa litawazawadi wachezaji wake wa soka pasipoti za kidiplomasia kwa kuishinda Romania 1-0 katika michuano ya Euro2016
Taifa la Albania limesema kuwa litawazawadi wachezaji wake wa soka pasipoti za kidiplomasia kwa kuishinda Romania 1-0 katika michuano ya Euro2016.
Taifa hilo halijashiriki katika mchuano wowote wa soka wenye tajriba ya hali ya juu.
Lakini haijulikani iwapo taifa hilo litafuzu kwa raundi ya pili nchini Ufaransa.
Timu hiyo itapewa zawadi zaidi ya Euro milioni moja pamoja na pasipoti hizo mpya,serikali imesema.
Albania ilipoteza mechi zake mbili na kuwa wa tatu katika kundi lake.
Waziri mkuu wa Albania Edi Rama alishuhudia furaha iliokuwepo nchini humo baada ya Armando Sadiku kufunga bao la kichwa na la ushindi dhidi ya Romania katika kipindi cha kwanza cha mechi.
Post a Comment