Baraza la Seneti Marekani lapinga hatua za kudhibiti silaha
Trump
Baraza la Seneti Marekani lapinga hatua za kudhibiti silaha
Baraza la Seneti nchini Marekani linalotawaliwa na wajumbe wa Republican limepiga kura ya kupinga mabadiliko manne ya sheria yaliyolenga kudhibiti mauzo ya bunduki na kupunguza machafuko yanayosababishwa na bunduki, baada ya mauaji ya watu 47 katika kilabu moja ya burudani wiki iliyopita mjini Orlando.
Ikiwa imesalia mwezi mmoja kabla ya wanachama wa vyama vya Republican na Democratic kuwaidhinisha rasmi wagombea wao wa uchaguzi wa rais, wabunge walishindwa kuweka kando misimamo yao ya kisiasa na kukubaliana kuhusu mojawapo ya masuala nyeti zaidi nchini Marekani. Hatua hizo nne, mbili kutoka kila upande wa chama, zingedhibiti uuzaji wa silaha, ikiwa ni pamoja na zinazonunuliwa na watu wanaoshukiwa kuwa magaidi.
Post a Comment