Header Ads

nyoka mkubwa

Nyoka mkubwa ambaye alikuwa akiishi katika dari ya nyumba moja nchini Australia kwa takriban miaka 10 sasa ameamua kuingia katika chumba cha kulala.

Mwenye nyumba hiyo Trina Hibberd kutoka eneo la Queenland aliamka siku ya Jumatatu na kumuona nyoka huyo mwenye urefu wa mita 5.2 amejipinda katika kitanda chake.

Aliwasha taa ya chumba hicho kabla ya mtaalam wa kushika nyoka Dave Goodwin kuwasili.

Bw Goodwin aliamua kumdunga sindano ya kulala nyoka huyo mwenye kilo 40 kabla ya kumuweka katika mkono wake na kuondoka naye.

Via>>BBC

No comments